Msanii wa nyimbo za injili, Enock Jonas ametishia kumshtaki mwimbaji wa lebo ya Wasafi, Zuchu kwa ukiukaji wa hakimiliki za wimbo wake maarufu sana uitwao ‘Wema wa Mungu’ au ‘Wema wa Mungu umenizunguka’ au ukipenda ‘Zunguka’ tu uliokua maarufu sana miaka ya nyuma.
Enock Jonas anaripotiwa kudai shilingi Milioni 500 za Tanzania ambazo ni kiasi sawa na zaidi ya Milioni 26 za Kenya baada ya kukiri Zuchu alitumia muundo na mbinu sawa na zake katika wimbo wake mpya ‘Kwikwi’ ambao unavuma na kufanya vizuri sana katika charts za muziki.
‘Wema wa Mungu’ ulitolewa mwaka wa 2012 nao ‘Kwikwi’ mwaka huu, 2022.
Kipande cha wimbo kilicho leta utata huu wote kipo katika dakika ya 0:49 ambapo msanii Enock Jonas anaimba maneno haya, “Zunguka, Zunguka, Zunguka, Zunguka, Zunguka, Zunguka,Zunguka, Zunguka yeeeh!”
Zuchu katika utunzi wake kwenye Kwikwi neno ‘Zunguka’ limetuka katika dakika ya 1:40 ila kuna tofauti kidogo katika mdundo na melody, hii inaweza kuwa kwa sababu umeimbwa katika key toufauti na ule wa Enock Jonas.
Kwa kiasi alichodai Enock, Milioni 500, meneja Babu Tale amesema itakua ngumu kulipwa hata Milioni 2 za Tanzania, kama malipo ya utumizi wa kionjo na mtindo wa wimbo wake.
Sheria za haki miliki katika nchi nyingi zinasema, ukiukaji unatokea pale zaidi ya asilimia 30% ya ubunifu umenyofolewa na kutumiwa, bila idhini ya mtunzi halisi wa kazi ya sanaa husika.
Binafsi, Enock Jonas anaweza kushinda kesi hii maana, ukisikiliza kazi zote mbili yake alafu ya Zuchu utasikia zimefanana ila asilimia zitatuliwa chini ya sheria za hakimili za Tanzania kama zipo wazi.
Hebu sikiliza nyimbo zote mbili kisha utoe kauli yako!