Mahaba niue! Wema Sepetu na Whozu, ndoa tunayo?

1 min read

Chimama na Chibaba, yaani kipenzi cha Watanzania, Wema Sepetu na Whozu wana jambo lao na mambo ni mengi sana, ila masaa ndiyo machache.

Wawili hawa wapo kwenye penzi zito, yaani kilichobaki ni mialiko ya kula biriani au ndoa InshaAllah.

Stori zilizokua zinaenea kwenye page za udaku kuwa wana familia upande wa Whozu na haswa mamake kuyakataa mahusiano yao ni uongo mtupu! Madai eti Tunda, mzazi mwenza na Whozu ndiye kipendacho roho zao pekee sio sahihi, eti Wema amekula chumvi kiasi cha haja sio hoja.

Liwe na liwalo, mapenzi yao yatazidi kuelea, wapambe kaeni chini.

Wema Sepetu anasema, “Kitu kimoja ambacho naweza kukisema ni kwamba mama mkwe ninampenda na ananipenda hivyo tu.”

Picha kwa hisani ya Instagram: Wema Sepetu

“Nimepitia maisha mengi sana, nimepitia maisha ya kusimangwa, ikafika muda nikaona kama nimekata tamaa, lakini kwa sasa hivi sina msongo wa mawazo, mbona kwa sasa hivi nipo sawa sana?”

Wema hajakua mwenye bahati katika safari zake za mapenzi, ila kwa Whozu amejizamia mzima mzima.

“Sihitaji msaada wa mtu yeyote tena nasema sihitaji msaada wa mtu yeyote, kwa sasa nipo sawa sawia,” ameongeza kusema.

Wema Sepetu ni mwigizaji wa filamu na mshindi wa tuzo za Miss Tanzania 2006.
Whozu naye ni msanii wa muziki.

Picha kwa hisani ya Instagram: Whozu

Ni kweli, barua ya moyo husomwa juu ya panda la uso! Hivi harusi tunayo hatuna?