Nafsi Huru – Darasa Huru lyrics

/
5 mins read

[Intro]

Yelaa Yelaaaa

Nananana Nafsi Huru Oii Rais Bila Ikulu’

 

[Verse]

Mwanafunzi wa maisha – Mkufunzi nafanikisha
itawapendeza wengi wakikuona unatembea uchi
haya usifiche uzae ushangae ilianza na muchi
mjini shule, mradi ule kakojoe ukalale
mitungi alele mikasi nyege usiache ikutawale
discipline is the key Nigga kuja polepole
Heshma wape wote Sonko, pia walokole
ukijipata kwa sokomoko vunga usiropoke
unakomaa kiukongwe usifananishwe na sokwe
Yote Tisa Who cares? Kote Ni visa Nightmares Bila kujali who stares
Unafanyiwa Vitu Don’t Dare, Bad Boys When they run up on you
What You Gonna Do- Shitstem ni ya Uduu
Get Rich or die trying kwa vijana ndio moto
MP ali get Rich wamekwama kwa msoto
kubadilisha destiny hawaogopi kuchoma photo
Usishangae Petty Thief amebeba cha moto
Preacher akila kwa Kristo Ngoko abonye za Sponyo
kukosa ni makosa ju ukikosa unazidi kosa
Tamaa ya kuosa wana force kua ma Boss Man
Social media floss na msosi tu unakosa
Ufurahishe Fake Friends, with fake hair na fake nails
Fake smile kwa fake face ukitafuta real Love na Fake style
Godamn – Unapojifanya mjanja ndipo unaonyeshaga ujinga
Roho safi unatoa wapi wakati una domo chafu
Wapambe, wanangoja urambe sakafu
Itawabamba ukiwa juu mradi sio ju yao
wenye gere na kwere zao wakoseshe mabao
Wakereke wakerekao dole la kati kwao
Wakiona sita ukiona Tisa Usibishane nao
Wenye mapepe wakerekete kwako wasilete zao
Nyama haifiki robo kilo ndio inazungusha dunia
in the line of duty wapo wazee walio angamia
Sahau kupata Fine ass ka hunaga finance
Utapoteza Finance ukikimbiza fine ass
Material World – Wife material ukiwahi – Lucky You
Huku kote ni ma Hood Rats utawapata kwa rat race
mapenzi ni ya ku purchase selling to the highest bidder
Inspired na waliopinda nafanya kitu napenda
less kusema more Kutenda inasonga calendar
Nashkuru Maulana Kila Manyana zikiachana Kope
Sarura sana watu around you hatoki mbali kupe
The more you give the More you receive
System ni nipe nikupe
Binadam ni kiumbe funny –
kuna yule utampa lift atake pia kupiga honny
Jasho umwage kuwabeba nawasengenye unavyo nuka kwapa ole wako ukichapa
Dogo ficha karata – kile Unataka zidi kutafata, Kile unapata shkuru unapata, leo ukihata
Kesho huta hata- Tumia Talanta kuzikamata – Lenga ma Hater zidi kupeta – Janta ni Janta we Furukuta – Uwe mafuta kama Kenyatta – Mambo swadakta hakuna matata – Walo kukataa watajileta – Wakijileta Unawakataa – Future better hupati ukiteta – Tatua Utata Usiwe Zezeta – Cheza smatter ku De Shatta, Keki ya taifa zidi kung’ata – zidi kunyata ukwepe disaster
Pesa Hufata Pesa Vile njaa uaga inafata Njaa
Kutesa unaeza tesa na uka Mess kama humjui Jah
Hujui ka Kesho ipo leo nilipo Moro sipo nitakapo kua
Lituapo jua nipigapo dua nipagapo
hatua nakuaga sure huezi ni zengua
mi na kalasua siezi sua sua
Acha inyeshe mvua – barka zianze tua – mimea ianze kua- ukisha mature ndio utagundua
Huezi muelewa Babako hadi nawe uwe baba
Ukim-let down mamako haachi kua mama
Kumbuka kosa moja hueza futa mema elfu akupendae kwa dhati ukaanza  mpa kichefchefu
piga hela ndefu ka ni heshima unataka ju kile unadhamini kwa mwengine ni takataka
mamlaka ukimwonjesha Kibaka atakuonyesha True colour hewala fanikisha maswala
Kulala – mwachie Marehem, pia marehemu alikua na mipango
jipange kabla hujapangwa – jibebe usingoje kubebwa – Jielewe usingoje kuelezwa
Utabebwa uanvyojibeba – ukiwaza we tekeleza –  Ukicheza ushindi kwaruza
Matusi usimtusi mamba kabla hujavuka mto
Zinduka Kitandani sipo zitimiapo ndoto
Kufuzu changa moto Hmmmm KImbiza ndoto
Siku zote pole pole ndio njia ya kufanya haraka kaka
Kubomoa ndio ujenge sometimes hukubalika Kaka
Kujikomboa muhimu walahi makinika Kaka Makinika Makinika
Siku zote pole pole ndio njia ya kufanya haraka dada
Kubomoa ndio ujenge sometimes hukubalika dada
Kujikomboa muhimu walahi makinika dada Makinika Makinika
Darasa Huru