Mohammed Ali exposes Joho badly Raila Odinga will not like this

///
9 mins read

Nyali MP Mohammed Ali insists that he will not stop exposing the rot in Mombasa politics and Kenya generally.

Moha says, he will not allow common people to be misrepresented by politicians and especially from the wealthy Joho family who seem to have a say in all decisions in Mombasa County.

During the August elections,Mohammed Ali of the Jicho Pevu fame beat Joho’s brother who was being pushed and favored by ODM after they allegedly rigged him out of the Raila Odinga led party.

This is what he says via his Facebook page:

Image result for mohammed ali joho raila

Lau kama jicho pevu la simba litafumba japo kesho, Je mtajua ukweli na uhakika wa uhalisia wa siasa za pwani na Kenya kwa ujumla? Wengi mumetaka kujua tofauti zilizopo kati yangu, Abubabakar Joho (ABUU) na Ali Hassan Joho Gavana wa Mombasa. Wanajigamba pwani kwa kudhalilisha watu hadi kufikia mmoja kujiita ‘mungu eti Alpha’. Wangapi matajiri wapo pwani na bado wanaheshima zao pasi kuwafanya wengine watumwa? Kwani cheo na pesa ndiyo tiketi ya kudharau na kukandamiza haki za wengine?. Tofauti zao kwangu na familia yao zilianza nilipohatarisha maisha yangu baada ya kuona wananchi wa kitaabika na kufariki kupitia jinamizi la madawa ya kulevya nilipofanya Makala ya upekuzi JICHO PEVU DAWA ZA KARAHA. Upekuzi ambao uliwaacha wengi vinywa wazi na kukumbatiwa kwa asilimia kubwa na Wakenya. Ripoti ya Saitoti ilitia huzuni familia ya ‘Alpha’ baada ya jina la Joho kuorodheshwa katika kikosi cha walanguzi wa dawa za kulevya nchini. Sasa hapa Mohammed Ali alionekana msaliti, mshenzi na adui kisa na maana upekuzi wake umewaletea shida. Kilele cha chuki zao kwangu ni pale walipopata taarifa kuwa mkombozi wa wanyonge Mohammed Ali ameingia katika ulingo wa siasa. Walitumia kila mbinu kuhakikisha ima najitoa katika eneo bunge la Nyali au nipiganie ubunge sehemu nyingine kama vile Jomvu au Changamwe. Juhudi zilipogongwa mwamba ndipo walipotangaza vita vya mitandaoni eti ‘Mimi si mpwani’, ‘Mimi nimemtenga babangu hata ya wao bila kujua alifariki mwaka wa 2007, ‘Mimi ni kibaraka’. Lakini walisahau mimi sikutumwa Nyali, mimi nazijua shida za Nyali na mimi sitanunuliwa kuisaliti azma, ari na ndoto ya kumkomboa mwana nyali. Kwa haraka alikimbia kwa ‘Baba’ Raila Odinga kwa lengo la kunipaka tope na kutaka usaidizi lakini alishtuka alipofahamu kwamba Raila anafahamu mchakato wangu wa kupigania haki. Raila anajua hatua nilizopiga kuangazia na kufichua mabaya. Ndipo Raila alimuambia “yule kijana ana kila sababu za kuwa mkombozi wacha tu kiongozi’’. Jibu hili lilimtoa upepo na hakuwa na lakusema ikijulikana fika alitaka ukuruba na Raila ndio ajipatie umaarufu na kujijenga kisiasa. Alimleta karibu Raila sio kwa kuamini falsafa na sera za baba bali kwa kujijenga kibinafsi akilenga kurithishwa mikoba ya Raila kwa ndoto yake ya mchana ya kutaka kuwa rais 2022. Pale kwa baba alikuta sisi ndio nguvu kazi na wapangaji wa “KIKAO” fursa iliyompa Raila nafasi ya kubadilishana mawazo huku akiuza mtazamo wake kila kaunti kwa vijana. Karata yake ya mwisho juu yangu ilikuwa nikuhakikisha sipati kiti cha ubunge wa Nyali kana kwamba wana nyali hawajui udhalimu, unyama na maovu inayowafanyia familia hiyo. Siku ya siku wakazi wa Nyali walisimama na haki na usawa na haki hii ilikuwa ni mimi Mohammed Ali ndio pale walilazimisha kunipokonya cheti cha ODM wakisahau wapiga kura walitaka mkombozi hawakutaka chama na hili lilidhihirika pale waliponipa ushindi ni kiwa kama mgombea wa kujitegemea. Lakini wacha niwakumbushe kitu. Mwakumbuka ile siku ya mkutano wa ODM Tononoka? Siku ambayo walitaka kunidhalilisha kwa kunisukuma na kuzuia nizungumze jukwaani? Basi wacha leo niwambie sababu ilikuwa ipi. Joho alitaka kila mgombea na kila mtu pia Raila Odinga kuvalia tisheti iliyo na jina lake. Kitendo kile sikukipenda hususan kwa mtu kama Baba ambaye historia yake ya kupigani haki na ukombozi kudunishwa kwa siasa za pesa nane. Nilimshauri Raila kutovaa fulana zile kwa kumpa sababu za kimsingi na mara moja alikubaliana nami. Kitendo cha Raila kuirudisha tisheti ndiyo kilichojenga uhasama na wakapanga njama ya kunidhihaki adharani lakini walikutana na Simba. Familia nzima pamoja na vibaraka vyao ilinizingira na kunizuia kuongea. Mkutano ulitibuka!
Alitarajia atanipanga kama alivyowapanga wale wagombea wengi Mombasa, Kilifi, Taita na Kwale katika uchaguzi wa mwaka 2017 kwa lengo la kuwatumia kufanikisha uovu wake akilenga wamuuzie sera zake za urais mwaka 2022, lakini alipofika kwangu alijua mimi si mtu wa ‘Shisha’ na ‘Selfie’ na huo utoto ni wa vichuzi wake na wala sio mimi. Siwezi uza utu wangu na wa mtoto wa Nyali kwa senti za haramu na dhulma. Joho sasa anadandia Raila akijitafutia uungwaji mkono wa kabila la Waluo akiamini tayari Pwani ipo mkononi mwake. Machoni mwa watu anapenda Raila lakini pembeni anakejeli Waluo mfano alikuwa wapi wakazi wa Owino Uhuru walipokuwa wanaatabika kule Jomvu? Mbona hakuna Mluo aliyefaidika katika serikali yake mwaka huu licha ya wajaluo kuwa wapigaji kura wakubwa Mombasa? Spika wa mwaka wa 2013 alikuwa Mjaluo kabla ya kufutwa kazi wa mwaka huu ni rafiki yake mpendwa na mtu aliyekamatwa na maafisa wa polisi mapema mwaka huu kwa tuhuma mbali mbali. Je, mnafahamu kwamba mwakilishi wa wadi mteule kwa vipindi viwili wameweka yaya wa nyumba yao? Huu ni uongozi ama ni unafiki? Tofauti ya Abu Joho, Ali Hassan Joho na Mohammed Ali ni hii. Mimi nilimpenda Raila Odinga na kujituma pasi na kusaidiwa huku nikitumia mshahara wangu, gari langu na nguvu zangu kuhakikisha safari hii ataibuka mshindi. Niliacha kazi yangu nikiamini kuwa tusipojitolea muanga na kujiunga na vuguvugu la tatu basi itakuwa hasara na vigumu kwetu kuikomboa Kenya tunayoitaka. Katika pilkapilka zangu kwenye siasa nilianza kuona mkono wa usaliti kutoka kwa familia ya Joho, lao kuu lilikuwa ni kutumia Raila Odinga ili apate umaarufu wa jamii ya wajaluo na kuonekana kama mrithi wa Raila Odinga baada ya siasa zake. Huku Raila Odinga akiendelea na kampeni Joho na Abuu Joho walikuwa wakifanya bidii na maadui zao kuunda serikali ya 2022. Joho na Evans Kidero walianza kumenyana kwa kutafuta ubabe wa kumrithi Raila Odinga badala ya kumsaidia. Watu wakaribu wa Raila Odinga wakiwemo mandugu wawili mmoja katika ofisi ya Raila na mwengine katika afisi ya Joho wakianza kutoa siri na mipangilio ya Raila. Wengine walikuwa wakipokea mshahara katika serikali hiyo hiyo iliyokuwa ikipingwa na Raila. Kila aliyejuu hushuka hata kama hataki. Joho anajua siri yake imetibuka. Wajaluo wamejanjaruka na Joho hana lake kuanzia sasa hadi 2022. Shida ya Abuu Joho na Joho ni Mohammed Ali, wanajua ninajua waliyofanya na nitamlipizia Raila Odinga kisiasa kama walivyomfanyia. Wanajua ninajua siri zao zote, wanajua siogopi ujinga, wanajua siabudu wao, wanajua nikianza kunguruma haki itapatikana Mombasa. Na sio wao pekee wanaonipinga na kunidhulumu kutumia vitoto vidogo vya mitandao na polisi wa CID, ninapigwa vita na watu wengine watatu Mombasa. Walanguzi wa dawa za kulevya, wezi na wanyakuzi wa ardhi. Wallahi naapa kwa jina la Mungu wala sio ‘alpha’ wa Mombasa kwamba nitatumia uhai wangu kupigania uhuru wa mpwani na Kenya kwa jumla wafurahi wakasirike lakini kwa imani na ushirikiano wenu siku njema inafika. Niwe Mbunge au nisiwe Mombasa haitamilikiwa na familia moja. Nikiwa hai kesho nitawaeleza mengi lakini hii ndio kauli yangu leo, nikifa kesho. Ashakum si Matusi!

Well,let the games begin…

Image result for mohammed ali joho raila